Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tory Lanez jela miaka 10 kwa kumuaa Megan Thee Stallion

Tory Lanez Ms Tory Lanez jela miaka 10 kwa kumuaa Megan Thee Stallion

Wed, 9 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa kutoka Canada #ToryLanez amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela, miezi saba baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga risasi msanii mwenzake #MeganTheeStallion na kumjeruhi miguu baada ya tafrija ya pool huko Hollywood Hills Julai 2020.

Jaji wa Mahakama ya Juu ya Los Angeles, David Herriford, alitoa hukumu hiyo Jumanne kwa Lanez mwenye umri wa miaka 31, ambaye alipatikana na hatia kwa makosa matatu: kushambulia kwa kutumia bunduki ya kivita, kuwa na bunduki iliyojaa (loaded), ambayo haijasajiliwa kwenye gari na kufyatua silaha mbaya. (uzembe).

Herriford alisema ilikuwa "vigumu kupatanisha" mtu mkarimu, mfadhili na baba mwema watu wengi walimtaja Lanez kuwa wakati wa kusikilizwa kwa hukumu na mtu aliyemfyatulia bunduki Megan Thee Stallion.

Ripoti zinasema Jaji huyo alimuhukumu Lanez kifungo cha miaka 6 kwa kushambulia kwa siraha na mingine minne zaidi juu ya kumiliki bunduki isiyosajiliwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live