Tory Lanez ni kama anajipanga tena upya kwenye Kesi yake ambayo imebakiza siku 18 pekee hukumu itoke, ambapo ni January 27 mwaka huu.
Taarifa zinaripoti kwamba Tory Lanez amemfukuza kazi Mwanasheria wake na kuajiri mpya (David Kenner) ambaye ana uzoefu mkubwa.
David Kenner anatajwa kuwawakilisha wasanii na watu maarufu kwenye Kesi zao kubwa ikiwemo ile ya Suge Knight, CEO wa zamani wa Label ya Death Row.
Lakini watalaamu wa masuala ya sheria wanasema, inaweza kuwa sio muda sahihi kwa Kenner kuweka mguu wake kwenye Kesi ya Tory Lanez kwani amechelewa sana, Kabla ya Mahakama kumkuta na hatia ndio ungekuwa muda mzuri zaidi.