Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tory Lanez Huenda Akatupwa Jela

Tory Lanez Tory Lanez

Thu, 4 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MWANAMUZIKI Tory Lanez huenda akatupwa jela kwa muda usiopungua miaka 23 ikiwa atakutwa na hatia ya kesi inayomkabili ya kumpiga risasi rapa wa kike kutoka nchini Marekani Megan Jovon Ruth maarufu Megan Thee Stallion.

Msanii huyo anadaiwa kumshambulia Megan kwa risasi mbili za mguuni Julai 2020 na waendesha mashtaka wamemtaka Lanez kufika mahakamani hapo kujibu shauri baada ya mwanamuziki huyo kufanya mgomo wa kuhudhuria kwenye kesi hiyo.

Kwa mujibu wa jarida la Rolling Stone la nchini Marekani, Tory Lanez atahitajika kufika mahakamani Disemba 14, 2021. Kulingana na sheria za Marekani, kwa kesi ya aina hii, adhabu yake huwa ni kifungo cha hadi miaka 23 jela endapo utapatikana na hatia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live