Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tofauti kati ya Diamond, Kiba na Harmonize ni hii

DIAMOND KIBAAAA Tofauti kati ya Diamond, Kiba na Harmonize ni hii

Mon, 1 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa muda kumekuwa sasa kumekuwa na gumzo kubwa kuhusu ni nani haswa mfalme wa muziki wa kizazi kipya Bongo baina ya bosi wa lebo ya Wasafi, Diamond Platnumz na gwiji wa mashairi ambaye pia ni mmiliki wa Lebo ya Kings Music, Alikiba.

Wadau wa masuala ya muziki wamekuwa wakibishana pasi na kufikia mwafaka kuwa nani ni mwamba katika tasnia hiyo, na kila mmoja amekuwa akivutia ngoma upande wake.

Sasa mdau mmoja wa masuala ya muziki Bongo, Hopeman David ameamua kuuanika ukweli na tofauti kati ya manguli hawa wa muziki ambao wamekuwa wakichuana kwa zaidi ya mwongo mmoja tangu wapate umaarufu katika tasnia hii.

Cha kushangaza ni kwamba msanii ambaye ni bosi wa lebo ya Konde Music Worldwide, Harmonize naye amejikuta akilinganishwa kwa namna moja ama nyingine na mahasimu hawa wawili wa tangu jadi.

David anasema, tofauti kati ya Harmonize, Diamond Platnumz na Alikiba ni wazi na kubwa kuliko jinsi watu wanavyofikiria na hata kufanay kufuru ya kuwalinganisha katika viwango sawa.

David anasema kwamba Alikiba ni msanii ambaye hapatawahi tokea kama yeye katika utunzi mzuri wa mashairi yaliyokwenda shule, lakini kilichomponza ni kwamba alishindwa kufanya muziki wake kuwa biashara, alichukulia poa sana katika kufanya muziki wake kuwafurahisha na kuwaburudisha mashabiki tu pasi na kujua kwamba muziki pia ni kazi na licha ya kuwa mtunzi mzuri, ipo haja ya kuufanya huo muziki kuwa biashara inayomuingizia kipato.

Kwa upande wa Diamond, mdau huyo anasema msanii Simba kinachomsaidia na kumweka kwenye gemu kwa muda mrefu ni ujanja wake tu, kwani msanii huyo anajua mbinu za kuufanya muziki wake upendwe hata kama hakuna cha muhimu anachokiimba.

David anasema Diamond anajua ujanja mwingi wa kuutangaza muziki wake kwa njia ya kibiashara kwa kuwekeza sana kwenye promosheni ya pesa nyingi kwa sababu anajua kwamba muziki kwake ni kama kazi na ambayo anaichukulia kwa umakini na kuuthamini zaidi ya kitu chochote.

Harmonize ambaye anawekwa katika viwango vya wawili hao ametajwa kuwa ni msanii aliyechipukia vizuri lakini ametekwa na kiki. Harmonize anasemekana kuwekeza sana katika kiki, jambo ambalo wengi wanahisi litauponza muziki wake sana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live