Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tiwa Savage, msanii pekee Afrika atakayetumbiza tamasha la King Charles III

Tiwa Savage, Msanii Pekee Afrika Atakayetumbiza Tamasha La King Charles III.png Tiwa Savage, msanii pekee Afrika atakayetumbiza tamasha la King Charles III

Wed, 3 May 2023 Chanzo: Radio Jambo

Tiwatope Savage, mwimbaji wa Nigeria, na mtunzi wa nyimbo anayejulikana kama Tiwa Savage, amechaguliwa kutumbuiza katika kutawazwa kwa mfalme ajao wa Uingereza, Charles wa III.

Tukio hilo muhimu limepangwa kufanyika katika kanisa la Westminster Abbey jijini London tarehe 6 Mei 2023.

Tiwa Savage atajiunga na watumbuizaji wengi nyota kwa ajili ya tamasha la kutawazwa na Big Lunch siku ya Jumapili, Mei 7, 2023.

Tiwa Savage ni mmoja kati ya waimbaji nane wanaoheshimika kutoka kote ulimwenguni ambao wamepewa fursa adimu ya kuvishwa taji la mfalme wa Uingereza huku Prince Charles Windsor akitarajiwa kutawazwa kuwa Mfalme mpya wa Uingereza.

Watumbuizaji hawa wengine ni pamoja na Steve Winwood, DJ Pete Tong, Lang Lang, Lucy, Paloma Faith, na Olly Murs.

Tiwa anatarajiwa kuweka historia ya kuwa msanii wa kwanza na pekee wa Afrika kutumbuiza katika kutawazwa kwa mfalme wa Uingereza.

“Nahitaji dawa na magari mawili ya kunibebea mabegi yangu, hata hivyo, London ninakuja. Hivi karibuni nitaandikisha historia na niko tayari,” Savage aliandika kwenye instastory yake baada ya kuteuliwa kupeperusha bendera Zaidi ya 50 za mataifa ya Afrika kwenye hafla kuu katika ardhi ya mkoloni.

Baada ya mama yake, Malkia Elizabeth II, kufariki, mfalme, Mfalme Charles III, na Malkia Consort, Camilla, watawazwa rasmi katika hafla hiyo ya kihistoria.

Waandaji walisema katika taarifa yao kwamba Tiwa Savage alichaguliwa kuwa miongoni mwa wasanii wachache ambao watatumbuiza katika tamasha hilo la kihistoria la kutawazwa.

“Tunayofuraha kutangaza kwamba Tiwa Savage atatumbuiza kwenye tamasha la kutawazwa pamoja na wanamuziki wengine wa kiwango cha kimataifa. Tiwa Savage ni msanii wa kipekee aliye na mchanganyiko wa kipekee wa sauti za Kiafrika na Magharibi. Tuna imani kwamba uchezaji wake utaongeza rangi na msisimko kwenye hafla hiyo,” taarifa hiyo ilisoma.

Wiki mbili zilizopita, tuliripoti kwamba msanii huyo alinusurika utekaji nyara nyumbani kwake ambao unaaminika kupangwa na dereva wake mpya.

Chanzo: Radio Jambo