Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tiwa Savage avutiwa na mavazi ya Ayra

InShot 20220530 141542371 Scaled Tiwa Savage avutiwa na mavazi ya Ayra

Wed, 29 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati mashabiki kutoka Nigeria wakimshambulia mwanamuziki Ayra Starr kuhusu mavazi yake yanayo onesha maungo ya mwili, kwa mwanadada Tiwa Savage imekuwa tofauti ambapo yeye anadai kuwa anavutiwa na mavazi hayo.

Akiwa katika mahojiano yake na Kiss FM, Uingereza, ameeleza kuwa tukio hilo linalo mtokea Ayra sasa linakumbusha enzi zake wakati anaanza mziki mashabiki nchini humo walipokuwa wakimnanga kuhusu uvaaji wake.

Lakini kwa upande wake anapenda uvaaji wa #Ayra huku akiyaona mavazi hayo ni ya kawaida na hayana shida yoyote inayopelekea awe ajenda kwa jamii.

AyraStarr na #TiwaSavage wamekuwa wakishirikiana katika kazi zao za Sanaa ambapo wawili hao waliwahi kuachi ngoma kama ‘Gala’ na ‘Stamina’.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live