Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Timu ya kushughulikia migogoro yaundwa baada ya kibao cha Will Smith

 Timu Ya Kushughulikia Migogoro Yaundwa Baada Ya Kibao Cha Will Smith Timu ya kushughulikia migogoro yaundwa baada ya kibao cha Will Smith

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: Bbc

"Timu ya kushughulikia mgogoro" itatambulishwa katika tuzo za Oscar za mwaka huu, ili kushughulikia matukio yoyote ya wakati baada ya tukio la Will Smith kumpiga Chris Rock wakati wa tuzo za mwaka 2022.

Mtendaji mkuu wa Oscars Bill Kramer aliliambia jarida la Time kitengo kipya "kimeendesha matukio mengi" kwa matumaini kuwa "watakuwa tayari kwa lolote". "Kwa sababu ya mwaka jana, tumefungua akili zetu kuwa mambo mengi yanayoweza kutokea kwenye tuzo za Oscar," alisema.

Sasa wako tayari kushughulikia hilo kwa harakaka , alisema. Rais wa Academy Janet Yang hapo awali alisema ugomvi wa Smith na Rock haukushughulikiwa haraka vya kutosha.

Smith alimpiga mchekeshaji Chris Rock baada ya kufanya mzaha kuhusu upara wa kichwa cha Jada Pinkett Smith, ambacho alikinyoa kufuatia kugunduliwa na ugonjwa wa alopecia.

Baada ya kurejea kwenye kiti chake, mwigizaji huyo alipiga kelele mara kwa mara, "Weka jina la mke wangu mbali na kinywa chako [cha uchokozi]" . Licha ya tukio hilo, alibaki kwenye sherehe hizo na baadaye akachukua tuzo ya uigizaji bora kwenye filamu ya King Richard.

Ingawa Smith baadaye alijiuzulu Oscars, ilichukua siku kadhaa zaidi kwa taasisi hiyo kufanya uamuzi juu ya uanachama wake. Hatimaye alipigwa marufuku kushiriki tamasha la Oscars na matukio mengine kwa miaka 10. Kramer alisema timu mpya itaweza kukusanyika "haraka sana" kutoa jibu usiku wa onesho lenyewe.

"Tuna tumaini kwamba hakuna kitu kitafanyika na kamwe hatupaswi kutumia [mipango] hii, lakini tayari tuna mifumo ambayo tunaweza kurekebisha."

Chanzo: Bbc