Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tiffah atamba kufanana na baba'ke, Diamond meno nje

Tiffah Na Baba Yake Tiffah atamba kufanana na baba'ke, Diamond meno nje

Mon, 26 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa Bongo Diamond Platnumz akiwa alifurahi baada ya bintiye na aliyekuwa mpenzi wake Zari Hassan, Tiffah Dangote kurekodi video akiongea na kuikarabati kuonyesha kana kwamba ana ndevu.

Katika video hiyo ambayo Diamond alipakia kwenye Instagram, Tiffah alisikika akijivunia kuwa anafanana na babake.

"Nafanana na baba yangu, amini hilo!" Tiffah alisema katika video hiyo ambayo ilirekodiwa kwa kutumia FaceApp.

Malkia huyo mwenye umri wa miaka saba alikuwa akizungumza na mama yake Zari kwenye video hiyo fupi.

"Hii ni sura ya baba" alimwambia. Zari alisikika akimueleza bintiye kuwa mwonekano huo wa sura yake uliokarabatiwa ni toleo lake jingine.

Tiffah ni mtoto wa kwanza wa bosi wa WCB Diamond Platnumz. Alizaliwa mnamo Novemba 6, 2015 wakati staa huyo wa bongo alikuwa kwenye mahusiano na Zari.

Katika kipindi cha mahusiano yao, wasanii hao wawili wa Afrika Mashariki walibarikiwa na mtoto mwingine mmoja pamoja, Prince Nillan ambaye alizaliwa Desemba 6, 2016.

Mara nyingi Diamond ameonekana kuwapendelea watoto wake na Zari zaidi ya watoto wake wengine wawili wanaojulikana. Mwanamuziki huyo ana watoto wengine pamoja na Hamisa Mobetto na Tanasha Donna.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live