Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tiffah asaini mkataba wa kutokuwa na 'boyfriend' mpaka afikishe miaka 30

TIFFAH MCHUMBA Tiffah asaini mkataba wa kutokuwa na 'boyfriend' mpaka afikishe miaka 30

Fri, 21 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Binti wa pekee wa staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz aitwaye Tiffah Dangote ametia saini hati ya kusihi asiwe na mpenzi hadi atakapofikisha umri wa miaka 30.

Tiffah ambaye ni mtoto mkubwa wa Diamond, alionekana kwenye video akiwa na kaka zake ambao walitoa ahadi yake ya kutokuwa na mpenzi hadi mwaka 2045 atakapokuwa na umri wa miaka 30.

Tiffah aliyezaliwa Agosti 6, 2015, ametia saini hati hiyo kabla ya kwenda kusalimiana na kaka zake kwa mtindo sawa na mikataba ya biashara.

"Siamini ni kaka zangu wanaonifanya nitie sahihi mkataba huu," Tiffah ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kuposti kipande cha video akisaini mkataba huo.

Hii inakuja ikiwa ni siku chache baada ya kumshangaza mamake Zari Hassan alipomwambia kuwa anataka kuwa video vixen na kucheza  kama wanawake katika video za muziki za babake Diamond Platnumz.

Tiffah ni miongoni mwa watoto wa watu mashuhuri ambao wana wafuasi wengi kwenye mtandao wa Instagram nchini Tanzania.

View this post on Instagram

A post shared by Latiffah ???????????????? (@princess_tiffah)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live