Mwanawe staa wa Bongo Diamond Platnumz na aliyekuwa mke wake Zari Hassan, Prince Nillan alisherehekea siku yake ya kuzaliwa mnamo Jumanne, Desemba 6.
Prince Nillan ambaye ni mtoto wa pili wa wanandoa hao wa zamani aliadhimisha miaka sita tangu alipowasili duniani.
Dadake mkubwa, Tiffah Dangote ni miongoni mwa waliochukua fursa ya kumsherehekea na kumtakia kheri njema ya siku ya kuzaliwa.
"Kwa squish wangu, rafiki yangu mpendwa, yule ninayeonyesha moto na shida nyingi, heri ya siku ya kuzaliwa Riaz," Tiffah alimwandikia kaka yake kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Tiffah aliambatanisha ujumbe huo na picha nzuri wakiwa pamoja na kujitambulisha kama "Malkia wa Tanzania."
Hapo awali Diamond Platnumz alimsherehekea mtoto huyo wake na kumhakikishia kuhusu upendo wake mkubwa kwake.
"Mwanangu wangu mtanashati alizaliwa leo. Mtoto wa mfalme, @princenillan," Alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Bosi huyo wa WCB huyo aliambatanisha ujumbe huo na picha ya mwanawe ambaye bila shaka ameendelea kukua kwa kasi kubwa
Katika ujumbe wake, staa huyo mkubwa wa Bongo pia alidokeza kuhusu kuumwachia zana zake za muziki.
"Baba anakupenda Nee, kua nikupasie kijiti," alisema.
Huku akimsherehekea mwanawe, Zari alimtakia Prince Nillan maisha marefu na kujivunia maendeleo yake.
"Kijana wenu mdogo ametimiza miaka sita leo, mnampenda aje sasa? Hapa kwa siku nyingi za kuzaliwa na baraka nyingi. Heri ya siku ya kuzaliwa ya sita Prince Nillan," alisema.
Nillan ni mtoto wa pili wa Diamond na mwanasoshalaiti wa Uganda Zari Hassan. Wapenzi hao wa zamani ambao wako na mtoto mwingine pamoja, Tiffah Dangote ambaye ana umri wa miaka saba.
Wazazi wenza hao walitengana mwezi Februari mwaka wa 2018 baada ya kuwa pamoja kwa takriban miaka minne.