Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tid: Media Ziligoma Kupiga Muziki Wangu

Mwanamuziki TID TID Mnyama

Thu, 10 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

TOP In Dar kwa kifupi TID; ni supastaa wa muziki wa RnB Afrika Mashariki akitokea nchini Tanzania ambaye anasema kuwa, kuna baadhi ya vyombo vya habari (media) ambazo ziligoma kupiga muziki wake kwa lengo la kuzima kipaji chake.

Katika mahojiano na Mtangazaji Salama Jabir, TID anasema kwamba, licha ya changamoto hizo ameendelea kufanya vizuri katika muziki.

Vilevile anaasema kwamba hulka yake ya kukosoa vituo vingi vya habari kuhusu namna ya kuendesha mambo yao, ilimchonganisha na watu wengi, jambo ambalo lilimsababishia kupoteza pesa nyingi ambazo angezipata kupitia muziki wake.

TID anasema licha ya kukosa kupanda jukwaani kwa muda mrefu, alifanikiwa kutafuta mbinu na biashara mbadala za kuleta chakula mezani, jambo ambalo anaamini linazidi kumfanya awe kidedea kwenye gemu la Bongo.

TID anaweka wazi kwamba kuna asilimia kubwa ya wasanii ambao amewashika mkono na hata kuwakutanisha na wasanii wakubwa ili washirikiane kwenye kazi za kimuziki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live