Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Thea acharuka: Marufuku kuniposyi siku nikifa

Batch 228725652 1627177584152384 996005310279277517 N Thea acharuka: Marufuku kuniposyi siku nikifa

Sat, 23 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Salome Ndumbagwe Misayo almaarufu Thea; ni mwigizaji wa kitambo kunako Bongo Muvi ambaye anasema kuwa, baadhi ya watu na hasa watu maarufu wana tabia mbaya ya unafiki.

Anasema kuwa, watu hao wanapoona mtu amekufa, ndiyo wanaanza kumposti mitandaoni, lakini hawakufanya hivyo alipokuwa hai kwani hawakumu-wish hata happy birthday.

Thea anasema kuwa, ameshangazwa mno kwenye msiba wa Maunda Zorro, watu wengi walimposti, lakini akiwa hai hakuna aliyewahi kuposti hata wimbo wake au yeye mwenyewe, jambo ambalo siyo sawa hata kidogo.

Thea anadai wasanii wengi ni wanafiki

“Nasema hivi, kama mimi hukuwahi kuniposti nikiwa hai, jamani mtu asije kuniposti nikifa kwa sababu kwangu mimi naona ni unafiki uliopitiliza kabisa, sasa unaniposti mimi naona kweli? Kwa kweli sitahitaji kabisa mtu atumie picha yangu kujiandikisha maneno ya hovyo,” anasema Thea

Chanzo: www.tanzaniaweb.live