Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

The Rock: Niliombwa nigombee Urais Marekani

The Rock Dwayne Johnson The Rock: Niliombwa nigombee Urais Marekani

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kulingana na chombo cha habari cha Variety, Mwigizaji Dwayne Johnson maarufu kama 'The Rock' alifichua kwenye kipindi kipya cha mchekeshaji Trevor Noah kinachojulikana kama "What Now?" kwamba vyama vingi vya kisiasa vilimfikia mnamo 2022 kumuuliza ikiwa angekuwa tayari kuwania urais.

Mwigizaji huyo alikuwa na wazo hilo katika mahojiano ya siku za nyuma, ingawa alisema mnamo Oktoba 2022 kuwa majukumu yake kama baba yatamzuia kugombea nafasi hiyo kubwa ya uongozi.

Katika mazungumzo yao, Noah alinukuu kura ya kisiasa ya 2021 (Poll voting) ambayo ilidai kuwa 46% ya watu wazima nchini Marekani wangemsaidia Johnson kwenye kampeni yake ya urais.

"Ilikuwa kura ya kuvutia ambayo ilifanyika na niliguswa sana na hiyo," The Rock aliongeza kwa kusema. "Nilishangazwa sana na nilihisi heshima kubwa. Nitashiriki kidogo hiki nawe: mwishoni mwa mwaka 2022, nilipata ziara kutoka kwa vyama vilivyoniuliza ikiwa ningekuwa tayari kugombea, na ikiwa ningeweza kugombea."

Unadhani The Rock anauwezo wa kuongoza taifa kubwa Duniani la Marekani Katika wadhifa wa urais au aendelee kukonga nyoyo za mashabiki wake katika kiwanda cha filamu tu? Tupe maoni yako.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live