Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

That Nigga Sugu is so great - Maloto

Sugu Samia Mnb That Nigga Sugu is so great - Maloto

Mon, 20 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwaka 1992, Enterprise Cinema, Mbeya, Sugu na BBG, wanazindua albamu “Machekibobu”. Kundi ni Niggaz To Public.

Mwaka 1994, Sugu akitumia moniker “2 Proud”, anatinga Yo Rap Bonanza kwa tiketi-jina “2 Proud and Dar Young Mob”. Alitoka wa pili nyuma ya Kwanza Unit. Akavunja tuzo kwa imani alionewa. Audience ilimsapoti mwanzo mwisho wakiamini alishinda.

Siku Yangu ni wimbo uliopokea waves za kutosha kutoka albamu “Ni Mimi” mwaka 1995. Hiyo ni albamu ya kwanza ya Sugu akiwa solo. 1996, albamu “Ndani ya Bongo”, 1997 “Niite Mr II”.

Negative opinions ziliibuka kila hatua ambayo Sugu alipiga. Alisemwa hajui kurap, but we grew up banging with his music. Club, radio, kwenye magari, disco vumbi hadi radio cassette za nyumbani, tuli-enjoy muziki wa Sugu.

Albamu “Nje ya Bongo” 1999, ilileta mapinduzi ya biashara. Mauzo kwa simu. 20 million shillings bank ndani ya mwezi. Wadosi wanaongeza mamilioni ili kupata haki ya kusambaza. Sugu anatoa sharti la mauzo kwa kugonga copy.

Sugu anabadili magari kwa fedha za muziki. Anafanya ziara Ulaya na Marekani. “Millenia” 2000 na albamu bora ya muda wote “Muziki na Maisha” 2001.

“Itikadi” 2002, “Sugu” 2004, “Coming of Age” 2006 na “Veto” 2009. Jumla albamu 10. Opinions zilezile negatives “Sugu si lolote!"

Sugu anaileta Bongo expensive crew, Lost Boyz 1998. Anawaunganisha major players wa Hip Hop katika Hip Hop Summit, Waterfront 2004.

2009 to early 2010, alitoa chozi alipodhulumiwa mchongo wa dola milioni 200 wa kampeni ya malaria, kupitia Malaria No More. 2010, akashinda ubunge Mbeya Mjini katikati ya vita kali.

Ubunge mihula miwili, akafungwa jela. Yupo nje ya Bunge, ila mabalozi wa Marekani wanapishana hotelini kwake Desderia, kumtembelea, kujadili issues. Kutoka Ambassador Don Wright mpaka Michael Battle.

Sugu akiwa Dar, utamwona vikaoni na mabalozi mbalimbali; Ufaransa hadi Ubelgiji. Sugu hit us by line “huwezi kuzuia mvua!” Ana-run entertainment na Bongo Flava Honors.

May 2022, Presidential Concert (The Dream), Serena Hotel. President Samia mgeni rasmi. That Nigga Sugu ambaye some pundits huponda “hana lolote”, anastawi sana. He’s so great. Let’s watch him carefully!

C&P Luqman Maloto

Chanzo: www.tanzaniaweb.live