Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tessy wa Aslay afunguka kuchumbiwa na mume wa mtu

Tessy Wa Aslay Tessy wa Aslay

Thu, 7 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mama wa mtoto wa msanii Aslay, Tessy akiwa kwenye mahojiano na moja ya chombo cha habari amekiri kwamba amewahi chumbiana na mwanamume ambaye alikuwa kwenye ndoa huku akidai kwamba wanaume kutoka Tanzania sio wa kujivunia nao.

"Nimechumbiana na mwanamume aliyeoa hapo awali. Wanaume wa Kitanzania sio wanaume unaweza kujivunia kujionyesha. Sikujua mwanzoni. Aliniambia baadaye kwa sababu alifikiri akiniambia nitamtupa.

"Hiyo ndiyo ilikuwa sababu mojawapo tuliyoachana. Niliondoka baada ya kujua. Iliumiza hisia zangu kwa sababu nilikuwa nampenda. Nilijiuliza ni siri gani nyingine anazohifadhi," amesema Tessy na kuongeza.

“Mahusiano yanaumiza na kumrudisha mtu nyuma, mimi nina moyo mwepesi sana na ni mwaminifu sana kwa watu, lakini wanaume wa Kitanzania sio waaminifu, wanaume wote niliotoka nao kimapenzi wanajua sijawahi kuwa-cheat, sijawahi kukaa kwenye mahusiano, kwa sababu hivi ndivyo wanaume walivyo," amesema Tessy.

Tessy alikiri kwamba Aslay amekuwa akimsaidia mwanawe na wala hajawahi mkana mtoto wake huku akiongeza kuwa kwa sasa yeye yupo singo (hana mpenzi).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live