Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tessy asimulia simu yake ilivyowaka moto ikiwa chaji

Tessy Asimulia Simu Yake Ilivyowaka Moto Ikiwa Chaji.png Tessy asimulia simu yake ilivyowaka moto ikiwa chaji

Tue, 11 Apr 2023 Chanzo: Radio Jambo

Mrembo Tessy Chocolate, ambaye ni mzazi mwenza wa msanii Aslay Isihaka amesimulia kitendo cha ajabu ambacho kilimtokea baada ya simu yake aina ya Iphone kulipuka na kuchomeka ikiwa kwenye chaji.

Tessy alipakia video ya simu hiyo ikiwa imeungua kabisa lakini pia ikiwa imeunguza hadi mto wa kitanda alilokuwa ameiweka juu ikiendelea kupata chaji.

“Jamani tusilale na simu ikiwa kwenye chaji. Hili limenitokea leo, simu ilikuwa kwenye chaji, imelipuka na kuwaka. Kumelipuka tumechanganyikiwa, ilikuwa kwenye chaji na huu ni mto,” Tessy Chocolate alisema akionesha madhara ya simu hiyo iliyokuwa imeungua kabisa pamoja na kuunguza mto.

Tessy ambaye walitengana na Aslay alisema kuwa tukio hilo lilitokea mwendo wa alfajiri ambapo alikuwa amelala kitandani na ndugu yake na pembeni mwake kulikuwa na simu yake ya Iphone ambayo ilikuwa imechomekwa kwenye chaji.

“Tulikuwa tumelala saa kumi na mbili asubuhi, na ndugu yangu. Yeye ndiye alikuwa amelala huo upande ambapo simu ililipuka, ni simu yake. Kilichotokea ni mlipuko halafu moto ukawa unatoka kama ule wa kupuliza. Ni kitu cha sekunde kama 30 hivi, kilitokea kwa haraka mno,” Tessy alisema.

Chanzo: Radio Jambo