Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tems awavuruga wazungu na gauni lake

E679a182c1b Tems awavuruga wazungu na gauni lake

Tue, 14 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa muziki nchini Nigeria, Tems amezua gumzo baada ya picha yake kusambaa ikimuonesha mmoja wa waalikwa wa Sherehe za Utoaji wa Tuzo za Filamu za #Oscars kushindwa kutazama mbele sababu ya vazi hilo.

Mwanamuziki huyo wa Nigeria amekosolewa vikali kwenye mitandao ya Kijamii baada ya kuvaa gauni lenye 'ngao' iliyowazuia wahudhuriaji wengine kuonekana na kuona mbele.

Gauni hilo jeupe lililokuwa na ngao iliyofunika kichwa chake, lilizua sintofahamu baada ya picha kusambaa ikimuonesha mwalikwa mmoja akikunja shingo yake ili kuweza kutazama jukwaani.

Watumiaji wengi wa Twitter walikerwa na kukosoa kitendo hicho kwa kumwita Tems "mkorofi", mwenye dharau na asiyejali wengine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live