Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tems apokea vitisho vya kuuawa kisa 'mimba' ya Future

Tems Futures Tems apokea vitisho vya kuuawa kisa 'mimba' ya Future

Thu, 14 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Temilade Openiyi, mwimbaji chipukizi wa Nigeria ambaye jina lake maarufu ni Tems, amefichua kuwa alipokea vitisho vya kuuawa kutokana na uvumi kuwa alikuwa na ujauzito wa rapa wa Marekani, Future.

Inaweza kukumbukwa kwamba alionekana akitingisha kile kilionekana kuwa kichanga kwenye onyesho la Wiki ya Mitindo ya Burberry's Spring/Summer London miezi kadhaa iliyopita.

Mshindi huyo wa Tuzo za Grammy ambaye hivi majuzi aliketi kwa mazungumzo na The Beat 99.9 FM, Lagos, alisema hakuwahi kufikiria kuwa kuna mtu yeyote angezingatia uvumi huo kwa uzito.

Kulingana na Tems, amesema watu walianza kumtumia meseji za vitisho na kumuuliza kwa nini anadaiwa aliamua kumpa ujauzito mtu kama Future.

Lakini mkali huyo wa ‘Try Me’ alifichua kuwa hajawahi kukutana na rapa huyo wa Marekani katika maisha yake licha ya kufanya kazi pamoja kwenye wimbo wake ulioshinda tuzo ya Grammy, ‘Wait For U’ pamoja na Drake.

Tems alisema: "Niliposikia [uvumi] kwamba nilikuwa mjamzito, sikufikiri kuna mtu yeyote aliamini. Sikujua ilikuwa mbaya hadi nilipoanza kupokea jumbe kama vile vitisho vya kuuawa, kama vile, ‘Unathubutu vipi? Kati ya watu wote ulimwenguni, Future, kweli?’ Na sijawahi kukutana naye maishani mwangu. Kwa hivyo ni wazimu."

Itakumbukwa kwamba mwanadada huyo alidai mtandaoni kuwa baada ya kumpata mpenzi wake na rafiki yake wa karibu wa miaka minane wamekuwa wakikutaka kwa siri na kusababisha mimba.

Katika video iliyosambaa mitandaoni, alisimulia jinsi alivyomtambulisha rafiki yake wa karibu kwa mpenzi wake kwani walikuwa watu wawili ambao walikuwa muhimu zaidi maishani mwake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live