Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tekno asaini emPawa africa

Tekno New Empawa 3 1000x600 Tekno asaini emPawa africa

Mon, 3 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii Tekno miles ameingia mkataba na kampuni ya emPawa africa katika kusimamiwa na kusambaza kazi zake za muziki, pia mkataba huo utamfanya Tekno kuwa m’bia wa kampuni hiyo (Share holder) katika msimu mpya wa kampuni hiyo.

Tekno ataungana na mtayarishaji wa muziki ambae ni mshindi wa tuzo ya Grammy “Michaël Brun” kuwa miongoni mwa watu waliowekeza katika kampuni hiyo ya emPawa Africa, kampuni hiyo ilianzishwa na msanii Mr Easy mwaka 2018 na lengo lake ni kusimamia kazi za wasanii wa barani afrika na kusaidia kupiga hatua zaidi katika maisha yao ya muziki.

emPawa africa imekuwa inazalisha vipaji vipya vya wanamuziki na kuvikuza na hawa ni baadhi ya wasanii wanaofanya kazi na kampuni hiyo ni pamoja na Joeboy, Fave, Dj neptune, King promise na wengine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live