Mama Diamond ni kama naye msanii tu maana unaambiwa naye alijua kusoma alama za nyakati kwa kunogesha shoo ya mwanaye baada ya yeye kuvamia jukwaa na kumkumbatia mwanaye.
Mpango mzima uli-happen kwenye jukwaa la Wasafi Festival pande za Mtwara jana Septemba 3, 2023 wakati Diamond alipokuwa akipafomu shoo ya marudio baada ya ile ya awali iliyofanyika juzi kukatishwa ghafla na hitilafu ya umeme.
Mama Diamond alivamia jukwaa pale mwanaye alipokuwa akipafomu wimbo wa Enjoy hususan pale kwenye anaimba 'kama kupendaaaa...bora nimpendea mama yangu..." mama akapanda, wakakumbatiana nakucheza pamoja hali iliyoibua shangwe la kutosha kutoka kwa mashabiki.