Mwigizaji wa pop wa Marekani, Taylor Swift amesifiwa kwa kutoa $5m (sawa na Tsh bilioni 13.625) kama msaada kwa waathirika wa kimbunga Helene na Milton.
Akielezea mchango wake kama "ukarimu", Claire Babineaux-Fontenot, ambaye anaongoza shirika lisilo la kifaida la Feeding America, alisema "utasaidia jamii kujenga upya, kupata chakula muhimu, maji safi na kujikwamua kutokana na dhoruba hizi mbaya" .
"Pamoja, tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli katika kusaidia familia wanapokabiliana na changamoto zilizopo.
"Asante, Taylor, kwa kusimama nasi katika harakati za kumaliza njaa na kusaidia jamii zenye uhitaji," Babineaux-Fontenot aliongeza.