Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taylor Swift amuidhinisha 'shujaa' Kamala Harris kuwa rais

Taylor Swift Amuidhinisha 'shujaa' Kamala Harris Kuwa Rais.png Taylor Swift amuidhinisha 'shujaa' Kamala Harris kuwa rais

Wed, 11 Sep 2024 Chanzo: Bbc

Mwanamuziki Taylor Swift amemuidhinisha Kamala Harris kuwa rais muda mfupi tu baada ya kumalizika kwa mjadala wake wa urais dhidi ya Donald Trump.

Katika chapisho la Instagram Jumanne usiku, nyota huyo wa pop alisema amefanya "utafiti" wake.

"Nitawapigia kura Kamala Harris na Tim Walz katika Uchaguzi wa Rais wa 2024," alisema. "Ninampigia kura @kamalaharris kwa sababu anapigania haki na kwa sababu ninaamini ninahitaji shujaa wa kuzipigania."

Swift aliendelea kumwita Harris "kiongozi thabiti mwenye vipawa".

"Ninaamini tunaweza kutimiza mengi zaidi katika nchi hii ikiwa tutaongozwa na utulivu na sio machafuko," aliandika.

Swift alitangaza habari hiyo pamoja na picha yake akiwa na paka na kutia saini "Childless Cat Lady", akimaanisha maoni yaliyotolewa na mgombea makamu wa rais wa Donald Trump JD Vance.

Seneta huyo wa Ohio amekabiliwa na msukosuko kutoka kwa klipu yavideo ya mwaka wa 2021 ambapo aliwaita wanachama kadhaa wa chama cha Democratic maarufu - ikiwa ni pamoja na Harris - "kundi la wanawake wanaomilikipaka wasio na watoto ambao wana huzuni maishani mwao".

Swift aliendelea kupongeza chaguo la Harris la mgombea makamu wa rais, Gavana wa Minnesota Tim Walz, ambaye alisema "amekuwa akitetea haki za watu wa mapenzi ya jinsi mojaLGBTQ+, IVF, na haki ya mwanamke kwa mwili wake kwa miongo kadhaa".

Mwimbaji huyo alisema kwa kiasi fulani alihamasishwa kushirikisha uamuzi wake wa kupiga kura na umma baada ya picha ya AI ya kumuidhinisha Trump iliyokuwa ya uwongo kuchapishwa kwenye tovuti yake.

"Iliongeza hofu yangu karibu na AI, na hatari ya kueneza habari potofu," alisema. "Ilinifikisha kwenye maamuzikwamba ninahitaji kuwa wazi sana kuhusu mipango yangu halisi ya uchaguzi huu kama mpiga kura."

Chanzo: Bbc