Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taylor Swift akataa kulipwa Bilioni 23

Tamasha La Taylor Swift Huko Seattle Lasababisha Mitetemo Ya Ardhi Taylor Swift akataa kulipwa Bilioni 23

Sun, 14 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa’ kutoka nchini Morocco French Montana amedai kuwa mwanamuziki na bilionea Taylor Swift alikataa kufanya show katika sherehe binafsi za Falme za Kiarabu ambapo aliahidiwa kulipwa dola 9 milioni sawa na tsh 23 bilioni.

Montana ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye mahijiano na #VladTV ambapo ameeleza kuwa mwezi Desemba mwaka jana alipokea ofa kwa ajili yake na Swift ili waweze kutumbuiza pamoja kwenye moja ya sherehe huko Uarabuni ambapo yeye alitakiwa kulipwa dola 1 milioni, lakini mwanamuziki huyo kutoka Marekani aliikataa ofa hiyo.

Aidha mpaka kufikia sasa bado haijafahamika sababu za Swift kukataa dau kubwa kama hilo, ikumbukwe kuwa mapema mwezi huu #TaylorSwift aliingia kwenye orodha matajiri wakubwa duniani.

Ambapo ametajwa kumiliki utajiri binafsi wastani wa dola 1.1 bilioni ikiwa ni sawa Sh 2.5 trilioni huku idadi hiyo ya fedha ikimfanya kuwa mtu wa 2,545 kati ya 2,781 ya mabilionea wa mwaka 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live