Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taylor Swift 'ahuzunika' baada ya shabiki kufariki kabla ya onyesho lake

Taylor Swift 'ahuzunika' Baada Ya Shabiki Kufariki Kabla Ya Onyesho Lake Taylor Swift 'ahuzunika' baada ya shabiki kufariki kabla ya onyesho lake

Sun, 19 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Taylor Swift amesema "amehuzunika" baada ya shabiki mmoja kufariki kabla ya tamasha lake huko Rio de Janeiro, Brazil, Ijumaa usiku.

Katika taarifa yake kwenye Instagram, mwimbaji huyo wa muziki aina ya pop amesema moyo wake "umeumia sana", na kuongeza: "Alikuwa mrembo na mchanga."

Hilo limetokea wakati halijoto ilipoongezeka katika jiji, ambalo ndilo kituo cha hivi punde zaidi kwenye Ziara ya Eras iliyovunja rekodi ya Swift.

Nyota huyo alionekana akiwapa mashabiki chupa za maji wakati wa tamasha hilo.

"Siamini ninaandika maneno haya lakini ni kwa moyo ulioumia kwamba nasema tulipoteza shabiki mapema usiku wa leo kabla ya tamasha langu," Swift aliandika.

"Siwezi hata kukuambia jinsi nilivyofadhaika na hili."

Swift alisema hangeweza kuzungumza juu ya tukio hilo akiwa jukwaani kwa sababu alihisi "kuzidiwa na huzuni" kila alipojaribu kulizungumzia.

"Nataka kusema ninahisi hasara hii ndani ya moyo wangu ulio na huzuni hadi kwa familia yake na marafiki."

Aliongeza kuwa hili lilikuwa "jambo la mwisho" alilofikiria lingetokea wakati akiwa ziara nchini Brazil.

Chanzo: Bbc