Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taxi Bubu ilivyomfikisha pabaya Adam Juma

Matonyambili 57336623 135595310902135 3798834724364761925 N Taxi Bubu ilivyomfikisha pabaya Adam Juma

Thu, 20 May 2021 Chanzo: eatv.tv

Leo ni 'Throwback Thursday' TBT hebu tujikumbushe wimbo wa Taxi bubu ambao Matonya alimshirikisha Fid Q, 'Video Queen' alikuwa Irene Uwoya na Director wa video ni Adam Juma.

Matonya ameshea stori hiyo kwa kusema Adam Juma aliondoka na gari yake bila ya ku-shoot kwa sababu alikuwa amefanyiwa 'Booking' ya mtu mwingine Tanzania ambapo wao walipanga ku-shoot Mombasa, hivyo akapiga simu 'Border' za mpakani kusema ameibiwa gari.

"Adam alikuwa amefanyiwa 'booking' ya mtu mwingine Tanzania hivyo anatakiwa akae siku moja tu Mombasa, akasema kesho lazima tu-shoot ili awahi kurudi, sisi tukasema haiwezekani lazima tuangalie Location na tukubaliane ndio tufanye kazi"

"Kuna kipindi Adam Juma hakuwa mzuri, alikuwa mjeuri mjeuri kidogo na mimi nikajitoa kwenye wema ambao ninao ndio tukafikia pabaya, Asubuhi akawasha gari akasepa, nikapiga simu kwenye boda zote na polisi nikawaambia nimeibiwa gari basi boda zote zikaekewa ulinzi, akakamatwa akawekwa Chumba geni akakaa kwa siku mbili" ameongeza

Kwa kuwa Chumba geni sio mbali na nyubani kwa kina Matonya hivyo Adam Juma akaomba mawasiliano na Mama mzazi wa Matonya ambaye alisaidia kumaliza tofauti zao na kutoka rumande.  

Chanzo: eatv.tv