Mwigiziaji maarufu nchini ‘Tausi’ amefunguka kuhusu tuhuma alizomkuta nazo dada wake wa kazi aliyekuwa akiishi nae kujihusisha na imani za kishirikina na kumuhusisha mtoto wake.
Tausi amesema ameishi na dada huyo kwa mwaka mmoja na miezi mitatu, huku akikiri dada huyo kuonyesha mapenzi ya dhati kwa mwanae na yeye alifurahishwa na upendo hup pasipo kujua mwanae anahusishwa kwenye imani hizo za kishirikina.
Ameongeza kuwa alifika kanisani na kutolewa uchawi huo uliopandikizwa na dada huyo wa kazi, huku dada huyo akikiri kujihusisha na imani za kishirikina mara baada ya kumuulizs ili kupata udhibitisho.
Aidha, Tausi amewanyamazisha wanaombeza kuwa mume wake mtarajiwa ni mfupi kama yeye huku akisema mume wake ni mrefu na hivyo watu watashangaa kumuona.