Muigizaji wa Filamu Bongo, Tausi Mdegela amefunguka juu ya changamoto na unyanyasaji anazokutana nazo mitandaoni, kazini pamoja na mitaani kutokana na muonekano wake ambao ni mfupi kwa kimo.
Tausi amesema kuwa kitu kinachomuumiza zaidi ni jinsi mwanaye wa kike anavyokuwa akitaniwa kisa muonekano wake.
Mbali na hivyo, Tausi anasema kuwa ana mwaka wa pili hajaitwa na muandaaji wa filamu yeyote kwa ajili ya kuigiza hivyo anajishikiza na biashara ili aendeleze maisha na mtoto wake.
Hata hivyo, Tausi ameongeza kuwa kumlea mtoto mwenyewe ni changamoto nyingine inayomkabili ila anajikaza kwani hapendi kuona mwanaye akiwa sio mwenye furaha.