Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tatizo tunamlazimisha Kiba afanye tunachokitaka sisi

Alikiba 79d0.png Alikiba

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Huwa nikimtazama AliKiba tangu arudi kwenye gemu mara ya pili tunamlazimisha sana atuelewe kuliko kumuelewa yeye, AliKiba ni msanii ambae tangu anatoka, alitoka katika kipindi ambacho sanaa zilikuwa zinaongea zaidi kuliko kiki.

Ukimzungumzia AliKiba sidhani kama kuna asilimia kubwa utaipata kuhusu maisha yake binafsi kuizungumzia kuliko muziki wake, kila mara amekuwa akiacha kazi zake ndio ziongee.

Sasa amekuwa akilazimishwa sana kufanya kile ambacho watu na Media zinataka ili wapige mpunga lakini amejitahidi kukaza japo kuna muda unaona kabisa anaanza kuachia.

Bifu lake na Diamond ukiachana wao kama wao kuwa na tofauti ambazo wanazijua wenyewe, Media nazo zimechangia pakubwa kuongeza tension. Nafikiri jamaa tungemwacha tu aendelee kutupa ngoma za kutuliza akili na ku enjoy.

Kwenye Compee huku tumpumzishe kwa sasa kijiti tumpe Konde Boy maana dogo anajua nini Media zinataka, ma pia anajua nini apige ili mseme alafu alipue mcheke alafu awanyee kabisa, kitu ambacho AliKiba kagoma.

Tumuache abaki kama alivyo ana ulimwengu wake, Huu Ulimwengu walikuwepo pia akina Rama Dee nao walipotaka kuendana na Media ndio wamepotea mazima.

Huu ulimwengu nauona pia kwa sasa kwa Dada Jide. Naye kwa sasa akitaka akazane na Media atapotea maana huu ulimwengu wa akina Nandy una balaa lake, wao waache Media zinawafuate wecnyewe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live