Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tasnia ya Urembo na Vipodozi Tanzania ilivyoathirika na janga la Corona

100012 Pic+vipodozi Tasnia ya Urembo na Vipodozi Tanzania ilivyoathirika na janga la Corona

Thu, 26 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tasnia ya urembo na vipodozi nchini Tanzania imeathirika sana na tishio la Corona nchini. Ingawa serikali imetangaza kufungwa kwa vyuo vikuu na mashule, maafisa wa afya bado hawajatoa miongozo au kuamuru vizuizi vyovyote kuhusu saluni za nywele, wakiwemo vinyozi, watengenezaji kucha, makeup artists nakadhalika.

Chama cha Urembo na Vipodozi Tanzania (TCA) wanasema wamejitahidi kutoa elimu ya kujilinda na virusi vya Corona kwa wanachama wake lakini wameona upenyo mkubwa uliopo ambapo elimu hii inapaswa kuwafikia wenye masaluni nchi nzima ili wafanyakazi wa masaluni na wateja wao wajue namna ya kujilinda na virusi vya Corona pamoja na kusaidia kuzuia kuenea kwa virusi hivi hatari. 

Akizungumza na Mwananchi, mwenyekiti wa TCA, Shekha Nasser ameonesha wasiwasi wake juu ya wenye masaluni kuweza kujimudu kifedha na familia zao ikiwa amri ya kufunga masaluni yote nchini itatoka.

 "Hatuwezi kumhudumia mteja kwenye masaluni kwa umbali wa mita moja wakati wa kumtengeneza kucha au nywele, ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa," alisema Shekha.

TCA imewaasa wanachama wake na wenye masaluni kote nchini kuchukua tahadhari.

Tasnia ya Urembo na Vipodozi ni moja ya sekta kubwa nchini iliyoajiri vijana wengi wa kike na wa kiume ambao vipato vyao vinategemewa katika kuhudumia familia zao kila siku.

Pia Soma

Advertisement
Virusi vya corona vinaathiri huduma, muda na fedha za wafanyakazi walio amua kujitenga “Social distancing” kwani njia kubwa ya kujikinga ni kulazimika kukaa nyumbani na kujitenga.

Nasser anasema TCA inawaomba wenye masaluni kote nchini kuvumilia, kuwa watulivu na kumuomba Mwenyezi Mungu kwani hali hii ni hatari sana na ni janga la dunia.

“Kama tulivyosikia maafisa wa serikali wametoa kote amri ya kuzuia msongamano wa watu kwenye mabaa, migahawa, sehemu za mazoezi, na biashara zingine ilikuzuia kuenea kwa COVID-19.

Hata hivyo watengenezaji wa nywele, kucha na wamiliki wa saluni bado hawajapigwa marufuku katika kazi zao hivyo wanalazimika kuamua wenyewe kuendelea kufanya kazi katika biashara zao huku wakichukua tahadhari na kufuata maelekezo ya wizara ya afya,” alisema Nasser. 

Kulingana na mwenyekiti huyo, kwa wale wenye masaluni walio amua kufunga, ni uamuzi ambao utakata chanzo chao cha mapato pekee kwa kile kinachoweza kuwa wiki  kadhaa au hata miezi ijayo.  

Saada Abdallah, mmiliki wa saloni Mikocheni, Dar es Salaam anakiri kwamba hawajapewa  maagizo maalumu ya kufunga.

“Lakini, namaanisha, kutokana na uelewa wa kila mtu, mahali pa kazi na mazingira yetu, ni, kama maeneo ya kuenea huu ugonjwa,”

Alisema wengine wanaamua kuendelea kufanya kazi hadi serikali au wizara ya afya itakapowalazimisha kufunga - na wanaendelea kufanya kile wanachoweza ili kudumisha usafi mahali pa kazi.

“Wengine wamechagua kufunga saluni zao kwa sasa kwa wasiwasi kwamba wanaweza kuwa wakichangia kuenea kwa ugonjwa huo wa Corona,” alisema Bi Saada Abdallah.

Chanzo: mwananchi.co.tz