Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tarehe ya Fiesta Dar yaanikwa

Fiesta Mlkn Tarehe ya Fiesta Dar yaanikwa

Fri, 4 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kusubiriwa kwa hamu, hatimaye Clouds Media Group leo imetangaza tarehe ya kufanyika kwa Tamasha la FIESTA 2022 jijini Dar es salaam kuwa ni December 3 katika Viwanja vya Leaders.

Taarifa rasmi kutoka Mjengoni leo @CloudsFMTZ ambayo haikutaja orodha ya Wasanii watakaotumbuiza, ilisomeka kwa maandishi machache yafuatayo;

"Dar es Salaam burudani imerejea nyumbani 88.5 MHZ DECEMBER 3 tunaweka maneno Leaders Club Kinondoni."

Wakazi wa Dar es Salaam waliikosa burudani ya kitaifa ya Dar es salaam kwa miaka mitatu mfululizo kwani Fiesta ya mwisho ilifanyika December 2019 kwenye viwanja vya Leaders.

Wasanii gani hautokubali wakosekane kwenye list? Wa nje au ndani ya Tanzania? Weka maneno kwenye comments.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live