Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzia: Muigizaji Gina Lollobrigida afariki dunia

Gina Lollobrigida Gina Lollobrigida

Tue, 24 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mcheza filamu maarufu duniani kutokea Italia, Gina Lollobrigida amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95.

Anajulikana sana baada ya kucheza filamu kama vile; The Hunchback of Notre Dame, Solomon and Sheba, Bread, Love and Dreams na nyinginezo. Alizaliwa Julai 4, 1927, huko Subiaco, Ufalme wa Italia.

Kulingana na ripoti ya shirika la habari la Italia, Lapresse, Gina Lollobrigida akifariki akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali moja huko Roma.

Gina ameacha mtoto wake Andrea Milko ambaye alijaliwa pamoja na mume wake wa zamani, Milko Skofic.

Mnamo Septemba mwaka jana, Gina alifanyiwa upasuaji wa kurekebisha mfupa wa paja uliovunjika wakati alipoanguka, alipona na kwenda kuwania kiti cha Seneti katika uchaguzi wa Italia ambao ulifanyika Septemba ila hakushinda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live