Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzia: Msanii Bongo Movie afariki kwa ajali

Chris Lubango.jpeg Chris Lubango.

Wed, 16 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Msanii wa Bongo Movie nchini Tanzania, Chris Lubango amefariki dunia wiki iliyopita baada ya kupata ajali ya gari nchini Marekani.

Lubango aliyekuwa anaishi nchini humo na kufanya kazi za udereva nchini humo amepata ajali hiyo akitokea Texas kwenda Chicago na kupata ajali katika Jiji la Oklahoma.

Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara ambaye yuko nchini humo amethibitisha taarifa za kifo hicho na kusema familia ya Lubango na Watanzania wanaoishi nchini humo wameanza taratibu za kuusafirisha mwili huo kurudi Tanzania kwa ajili ya shughuli za maziko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live