Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzia: Malu Stonch wa FM Academia afariki Dunia

Malu Stonch 2876998 Tanzia: Malu Stonch wa FM Academia afariki Dunia

Sun, 7 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwimbaji nyota wa FM Academia, Emery Malu Stonch amefariki dunia ikiwa ni muda mchache baada ya kuanguka ghafla jukwaani akiimba katika onesho la Bendi hiyo.

Malu Stonch alianguka na kupoteza fahamu wakati alipokuwa akiwajibika katika ukumbi wa Target uliopo Mbezi, Beach, jijiji Dar es Salaam usiku wa Jumamosi Aprili 7, 2024 wakati akiimba wimbo wa "Hadija".

Taarifa za wadau zinasema baada ya kupatiwa huduma ya kwanza akakimbizwa Hospitali ya Masana ambapo alihamishiwa Lugalo ambapo ilithibitika kuwa Stonch tayari alikwishafariki.

Mwanahabari na mdau mkubwa wa muziki, MC Petit aliyekuwa miongoni mwa waliomkimbiza Malu Stonch hospital, ameithibitishia Saluti5 kuwa mwimbaji huyo amefariki.

"Pale Masana walipompokea tu, wakatumbia tumpeleke Lugalo Hospital kwa kuwa mgonjwa wetu ameshafariki," ameeleza MC Petit.

"Tulipofika Lugalo nao wakatuthibitishia kuwa Malu Stonch amefariki na hivyo tukafanya utaratibu wa kumpeleka chumba cha kuhifadhi maiti," alifafanua zaidi MC Petit.

Pumzika kwa amani Malu Stonch.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live