Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzia: Erick Kisauti afariki dunia

Erick Msanii Erick Kisauti afariki dunia

Wed, 17 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchekeshaji Sobogani Zabron ‘Erick Kisauti’ wa Vituko Show iliyokuwa inaruka katika Luninga ya Channel Ten, amefariki Dunia leo Agosti 17, 2022.

Taarifa zilizothibitishwa na msanii mwenzake wa vichekesho, Tiny White, zinaeleza kuwa msanii huyo amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Tiny White amesema asubuhi ya leo alipigiwa simu na ndugu wa karibu wa Erick na kumpa taarifa za kifo chake.

Ameeleza kuwa Erick alikuwa mgonjwa ambapo hapo jana aliwasiliana naye na kumueleza kuwa alikuwa amevimba mwili mzima.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live