Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yatinga fainali CECAFA

Final Pic Data Tanzania yatinga fainali CECAFA

Wed, 28 Jul 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

TIMU ya Tanzania chini ya miaka 23 imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya kombe la CECAFA kwa vijana baada ya kuifunga Sudan Kusini bao 1-0, katika hatua ya nusu fainali mchezo uliopigwa katika uwanja wa Bahir Dar nchini Ethiopia.

Tanzania ilijipatia bao pekee kutoka kwa Kelvin Nashon dakika ya 64 baada ya kupiga faulo nje ya 18 iliyomshinda mlinda mlango wa Sudani Kusini na kutinga wavuni moja kwa moja.

Katika mchezo huo ulikuwa wa kuva ni kuvute kwa timu zote mbili kushambuliana kwa zamu huku Tanzania ikionekana kuwa na utulivu katika eneo la kujilinda kwa kuzuia mashambulizi ya Sudani Kusini hali iliyowapa wakati mgumu wapinzani hao kutoka Juba.

Ushindi huo unaifanya timu hiyo inayonolewa na kocha Kim Poulsen kuendelea kufanya vizuri baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya DR Congo katika mchezo wa awali kabla ya kutoka sare ya kufungana kwa bao 1-1 dhidi ya Uganda katika hatua za makundi.

Tanzania imetinga fainali ya michuano hiyo ya vijana huku ikimsubiri mshindi kati ya Kenya au Burundi, huku fainali ya michuano hiyo ikitarajiwa kufanyika Julai 30 katika uwanja wa Bahir Dar nchini Ethiopia.  

IMEANDIKWA NA DAUDI ELIBAHATI

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz