Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania mwenyeji Mashindano ya Viziwi Afrika

Kiziwi Mbele Mbele Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa, Leah Kihimbi

Tue, 28 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya Urembo na Mitindo kwa Watu Wenye Usikivu Hafifu (Viziwi) Bara la Afrika yatakayofanyika Oktoba Mosi, 2021 katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika Mkutano na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa, Leah Kihimbi amesema kuwa maandalizi ya mashindano hayo tayari yamekamilika na sasa Washiriki kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wamewasili nchini na sasa wanaendeleo ya mazoezi yanayofanyika uwanja wa Mpira wa Mkapa Jijini Humo.

“Mashindano haya yanaandaliwa na kuratibiwa na Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo pamoja na Kituo cha Sanaa Utamaduni kwa Viziwi Tanzania (KISUVITA) yakihusisha vijana wa kike na wa kiume ambao wengi wao tayari wamewasili jijini Dar es Salaam kujiunga na kambi ya maandalizi kuelekea mashindano hayo kuanzia Septemba 24 hadi 30, 2021" amesema Kihimbi.

Kihimbi amesema kuwa kutokana na Umaalumu wa kundi hili, kimkakati mashindano haya yataitangaza Tanzania kimataifa, ikizingatiwa kwa sasa Tanzania inaendelea kujipambanua kama nchi inayojali na kuthamini watu wote bila kujali changamoto zao za kimaumbile.

Mashindano hayo yanaongeza chachu na kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kupitia programu maalumu ya kuitangaza nchi yetu kimataifa ijulikanayo kama “Re-branding Tanzania”, ambayo inalenga katika kutangaza fursa za utalii na uwekezaji nchini.

Kwa upande wake Rais wa Sanaa na Utamaduni kwa Viziwi Barani Afrika, Habibu Mrope, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kukubali kufanikisha mashindano hayo na kugharamia malazi, chakula, usafiri wa ndani wakati wote wa mazoezi ya washiriki hadi mwisho wa mashindano hayo ambayo yatahitimishwa Oktoba 1, 2021, Serena Hotel Jijini Dar es Salaam.









Washiriki wa Mashindano ya urembo na mitindo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live