Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania kuwa mwenyeji wa Miss Africa Golden 2022

Mag1 Washindi wa Miss Africa Golden

Mon, 31 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuwa wenyeji kwa mafanikio wa fainali za dunia za Miss Tourism Worlds 2006, kupitia Miss Touirism Tanzania Beauty Pageant LTD kampuni tanzu ya Africa Tourism Promotion Centre ,Tanzania imepewa tena heshima ya kuwa wenyeji wa fainali za dunia za Miss Africa Golden 2021/2022. Fainali za dunia za Miss Africa Golden 2021 / 2022, zitashirikisha zaidi ya warembo hamsini (50) wenye mataji ya kitaifa kutoka zaidi ya nchi hamsini duniani kote.

Tarehe kamili ya kufanyika kwa fainali hizo ,itatangazwa na Rais wa dunia wa shindano hilo SAPPHIRE ADAOBI OBI katika mkutano wa kimataifa na waandishi wa habari utakao fanyika mapema mwezi Februali , 2022 jijini Dar Es Salaam, baada ya kukamilisha taratibu na kanuni za kiserikali na mamlaka zake. Hata hivyo inatatarjiwa fainali hizo kufanyika kati ya mwishoni mwa Februali na Machi 2022.

Miss Africa Golden World, ni shindano kubwa zaidi duniani la urembo, linaloshirikisha warembo kutoka nchi zote duniani wenye asili ya kiafrika, huku fainali za mwaka huu zikiwa ni za nne tangu kuanzishwa kwake.

Tayari nchi zaidi ya arobaini (40) zimethibitisha kushiriki fainali hizo za dunia , ambazo zitafuatiliwa katika mabara yote duniani kupitia vyombo mbalimbali vya habari vya kielekroniki ,machapisho na mitandao ya kijamii, lakini pia kuangaliwa mbashara duniani kote kutokea katika viini vya vivutio vya utalii ,uwekezaji na utamaduni vya Tanzania bara na Zanzibar kupitia matangazo ya Televisheni na mitandao ya kijamii.

Miongoni mwa nchi zilizo thibitisha kuja Tanzania kushiriki fainali hizo ni pamoja na :

Austria, Cameroon, Nigeria, Nigeria, Ghana, Sudan, Nigeria, Swaziland, Colombia, Turkey, Ethiopia, Somalia, South Sudan, Mauritius, Ghana, Rwanda, Benin Republic , Zambia, Haiti, Uganda, Dominican Republic, Nigeria, Australia, Uganda, Zimbabwe, Botswana, Namibia, Haiti, Cameroon, Mozambique, Sierra Leone, South Africa, Gambia, Austria, Benin, Burundi, Guinea, Kenya, Canada, France, Germany, India, Montenegro, Angola, Japan, Russia, United Kingdom, Malawi, United State of America, Greece, Spain, Tanzania etc

Wakiwa nchini,washiriki wakiambatana na waandishi wa habari za televisheni, redio, magazeti ,mitandao ya kijamii, wapiga picha za video na minato , watafanya ziara za promosheni katika vivutio vya utalii,utamduni,huduma za misitu, hifadhi za bahari, wanyama pori, mazingira, uwekezaji, maliasili nyingine za taifa na meneo ya vipaumbele vya serikali na wadhamini wakipiga picha za matangazo, vyombo vya habari na mitandao ya kijamii , huku wakitangaza na kuhamasisha utalii, utamduni, uwekezaji, uhifadhi, maendeleo ya kijamii na kiuchumi mijini na vijijini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live