Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania kupewa uenyeji Jamafest 2032

77107 TANZSANIA+PIC

Wed, 25 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akitarajiwa kufunga Tamasha la Jumuiya ya Afrika Mashariki Utamaduni Festival (JamaFest) Septemba 28, 2019, Tanzania itaandaa tena mwaka 2032.

Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuandaa tamasha hilo tangu lianzishwe mwaka 2011 na linafanyika kila baada ya miaka mwili kwa kuzunguka kwenye nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki.

Mwenyekiti wa Taifa wa kamati ya maandalizi, Joyce Fisso amesema baada ya uenyeji wa msimu huu Tanzania itapewa uenyeji mwaka 2032 baada ya kufanyika kwenye nchi nyingine kila baada ya miaka miwili.

"Tamasha limekuwa likizunguka kwenye nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki, lilianzia Rwanda, Kenya, Uganda na msimu huu limefanyika Tanzania,".

“Litaendelea kufanya hivyo hadi mwaka 2032 litakaporudi tena hapa nchini, huwa linafanyika kila baada ya miaka miwili, ”amesema.

Amesema mwamko umekuwa mkubwa kwani walitarajia vikundi 26 kushiriki, lakini vilivyojitokeza ni zaidi ya 40.

Pia Soma

Advertisement
"Tumefanikiwa kuliandaa kwa kiwango bora, tumeitangaza Tanzania na utamaduni wa Jumuiya ya Afrika Mashariki," amesema.

Amesema katika hafla ya kufunga tamasha hilo, watatangaza nchi itakayokuwa mwenyeji na itakabidhiwa bendera ya uenyeji.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz