Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Tanzania kupeleka sita 'Miss & Mr deaf' Brazil

33b654b5f4359f31a4ee5f49530b0692.jpeg Tanzania kupeleka sita 'Miss & Mr deaf' Brazil

Sun, 3 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TANZANIA imepata nafasi ya kupeleka washiriki sita katika Fainali za Urembo, Mitindo na Utanashati kwa Viziwi ngazi ya Dunia zilizopangwa kufanyika April 2022 nchini Brazil.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, imenukuu maamuzi ya Kamati ya Kimataifa ya Mashindano hayo kuwa washiriki wengine wanne kutoka Tanzania wataungana na washindi wawili wa awali wa mashindano ya aina hiyo kwa Afrika yaliyofanyika Dar es Salaam Oktoba Mosi.

Khadija Kanyama aliyeshika nafasi ya pili Afrika (Kundi la Deef Afrika 2021) na Carolyne Mwakasaka aliyeshika nafasi ya kwanza (Kundi la Miss Deaf Afrika – Mitindo) walipata nafasi ya moja kwa moja. Hata hivyo, Surath Mwanis, Rajani Ali na Russo Songoro (walioshiriki upande wa Mavazi na Mitindo) na Joyce Denis (eneo la Urembo) nao watashiriki fanali hizo.

Makamu wa Rais wa Mashindano hayo Artur Dzerbis ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuandaa mashindano ya aina hiyo yaliyoshirikisha nchi 13 kutoka Bara la Afrika kwa mara ya kwanza katika viwango vya juu.

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Hassan Abbasi amesema Tanzania ipo tayari kuendelea kuandaa mashindano ya Bara la Afrika kwa miaka mingine mitatu na kuomba Kamati ya Kimataifa ya Mashindano hayo kuridhia ombi la Tanzania.

Chanzo: www.habarileo.co.tz