Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanasha ampa tano Diamond

35104db069dd1a171c814ac2fb7c4bd1 Tanasha ampa tano Diamond

Mon, 21 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MZAZI mwenzie na Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna amesema anajivunia kuona Diamond akimhudumia mtoto wao.

Akizungumza akiwa nyumbani kwao Kenya, Tanasha alisema kwa sasa anaona jitihada za Diamond katika kumhudumia mtoto wao tofauti na hapo awali.

“Kwa mwanaye kwa sasa anafanya jitihada za kumhudumia kwani analipa ada ya shule. Kile anachofanya kwa mtoto wake, nakipenda, anafanya jitihada kuwa baba mzuri, ninajivunia,” alisema.

Aidha Tanasha alisema nyumba aliyonunua hivi karibuni ni kwa fedha zake mwenyewe na hajapewa fedha na Diamond bali.

Wawili hao waliachana mapema mwaka huu baada ya kujaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwae Nassib Junior na kufanya muziki pamoja.

Chanzo: habarileo.co.tz