Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanasha amchamba jirani wa mama'ke

Tanasha Donaaaa Tanasha

Wed, 31 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki maarufu kutoka Kenya, Tanasha Donna yuko nchini Ubelgiji ambako anafurahia wakati na mama yake.

Katika siku za hivi majuzi, mpenzi huyo wa zamani wa staa wa Bongo Diamond Platnumz amekuwa akitumia ukurasa wake wa Instagram kupakia picha na video zake akiwa katika nchi hiyo ya Ulaya.

Jumatatu alipakia video inayoonyesha akiwa nje ya nyumba ya mamake na kufunguka kuhusu jirani wa mamake ambaye alimshtumu kwa kuwa mbaguzi wa rangi

"Acha niwaambie kitu cha kushangaza. Jirani wa mamangu ni mbaguzi wa rangi waziwazi. Hapendi watu weusi na hata huwa hajaribu kuficha.

"Kila wakati familia ama marafiki wanapokuja huwa hajaribu kuficha," Tanasha Donna alisema katika video ambayo alipakia kwenye Instastori zake.

Mama huyo wa mvulana mmoja alifichua kuwa jirani huyo wa mamake hata hivyo anamiliki farasi mweusi.

Tanasha alishangaa jinsi jirani huyo alivyochagua kuwa na farasi mweusi ilhali anawachukia waziwazi watu weusi. "Hupendi watu weusi lakini hujali kuwa na farasi mweusi. Huo ni upuuzi," alilalamika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live