Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanasha: Sipendi mwanangu awe kama Diamond

Diamond Tanashaaa Tanasha: Sipendi mwanangu awe kama Diamond

Sat, 30 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwimbaji na mwanamitindo maarufu wa nchini Kenya, Tanasha Donna ameweka wazi kuwa matamanio yake ni mwanaye Naseeb Juniour kuwa mwanasoka na si kuwa mwananamuziki kama alivyo baba yake mzazi Diamond Platnumz.

"Kama mama yake ni mwimbaji na baba yake ni mwimbaji. Kuna uwezekano mkubwa wa yeye kufuata njia hiyo, Mungu pekee ndiye ajuaye. Ingekuwa kwa matakwa yangu, ningemtaka awe mwanasoka," Tanasha alisema.

Mpenzi huyo wa zamani wa Diamond alibainisha kuwa kimsingi, wanamichezo huwa na nidhamu sana tofauti na wanamuziki.

"Najua watu wanaojihusisha na michezo wana nidhamu sana. Wanaamka mapema, wanafanya mazoezi, wanakimbia, hawanywi pombe kwa sababu kuna vipimo vinavyofanywa kila wakati. Ingekuwa uwezo wangu, ningetaka hivyo kwa sababu tasnia hii ya muziki inakuja na mengi. Kuna siasa nyingi nyuma yake.

"Kuna mengi ambayo hufanyika katika tasnia ya muziki. Ukiwa una ushawishi na pesa nyingi, unaweza kuendesha mambo mengi. Ndivyo hukuwa kwenye tasnia nyingi. Hata hivyo naamini kila tasnia huja na mazuri yake na mabaya yake. Hata michezo huwa na upande wake mbaya," alisema Tanasha.

Tanasha hata hivyo alidokeza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa mwanawe huyo kufuata nyayo zake na Diamond na kwamba ikitokea Naseeb Jr awe mwanamuziki basi hatasita kuunga mkono taaluma yake na kumsaidia kuikuza.

"Lakini ikitokea afanye muziki nitamuunga mkono kikamilifu na nitakuwa na uzoefu wa kumwelekeza katika njia sahihi. Acha tuone, muda utasema," alisema Tanasha.

Hivi majuzi wakati Tanasha alikuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa, Naseeb Juniour alitengeneza video akisherehekea birthday ya mama yake. Mtoto huyo mwenye umri wa miaka miwili alirekodi wimbo wa kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa mama yake kwa sauti nzuri. Naseeb ni mtoto wa pekee wa Tanasha na mzaliwa wa nne wa staa wa Bongo Diamond Platnumz.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live