Tanasha Donna; ni mwanamama wa Kenya anayefanya muziki wa Kizazi Kipya ambaye alipata umaarufu zaidi baada ya kuchumbiana na supastaa wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz.
Tanasha na Diamond wana mtoto wa kiume, Naseeb Junior. Hata hivyo, Tanasha na Diamond walitengana miezi michache baada ya kubarikiwa mtoto huyo.
Tanasha amefichua kuwa mwaka 2022 uhusiano pekee anaotaka kuurekebisha ni uhusiano wake na Mwenyezi Mungu.
Tanasha anaonekana hajajiandaa kuendelea na mtu mwingine bado baada ya kuachana na Diamond. Tanasha anasema; “Uhusiano pekee ambao nataka kuurekebisha, ni uhusiano wangu na Mungu.”