Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tamko la Basata kwa wasanii wanaogombea Ubunge

FA Tamko la Basata kwa wasanii wanaogombea Ubunge

Mon, 29 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la Sana la Taifa (BASATA) wamesema hawana tatizo na wasanii wote wanaogombea Ubunge kwani ni moja wapo ya fursa na wanataka waichangamkie vyema ili waweze kuwa Wabunge.

Akizungumzia hilo Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza ameeleza kuwa "Wasanii wachangamkie fursa ya kuwa Wabunge, wapo wasanii wengi ambao wapo Bungeni kama Prof Jay na Joseph Mbilinyi "Mr II Sugu", msanii atakayezungumzia changamoto za wasanii kwenye muhimili wa Bunge ndiyo msanii tena nitapata faraja kweli, katika hili Basata tunawapongeza sana wasanii ambao wanaonyesha nia katika kugombea uongozi ni haki yao ya msingi"

Mpaka sasa wasanii waliotangaza nia ya kutaka kugombea Ubunge kwenye uchaguzi mwaka huu 2020 ni Mwana Fa (Muheza,Tanga), Shilole (Igunga Tabora), Baba Levo (Kigoma Mjini), Steve Nyerere (Iringa Mjini) na Wakazi (Ukonga, Dar Es Salaam).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live