Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tamasha la Urithi Karatu lafana, Dk Mwakyembe kunoigesha zaidi

80929 Pic+tamasha Tamasha la Urithi Karatu lafana, Dk Mwakyembe kunoigesha zaidi

Mon, 21 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Karatu. Mamia ya wananchi wilayani hapa wanashiriki Tamasha la Urithi ambalo Jamii za makabila ya Datoga, Hadzabe, Iraqw na Maasai wanaonyesha tamaduni zinazohusu maisha yao ya kila siku.

Tamasha hilo ambalo limeingia siku ya pili leo Jumamosi Oktoba 19,2019 limevuta wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi kujifunza jamii hizo zinazotajwa kuendelea kutunza mila na tamaduni zao kwa miaka mingi.

Katibu Tawala Msaidizi Huduma za Jamii mkoa wa Arusha, Agnery Chitukulo amesema tamasha hilo linalenga kuwaleta watu pamoja kujifunza utajiri uliopo nchini na linatumika kuwalenga watalii kuongeza idadi ya siku za kuwepo hapa nchini.

“Tunataka jamii iendelee kurithisha mila na desturi zetu kwa watoto wao katika nyanja tofauti za maisha na kuhakikisha watalii wanaongeza siku za kukaa nchini ili kuongeza mapato yanayotokana na sekta ya utalii,” alisema Chitukulo

Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya maandalizi ya Tamasha la Urithi, Martin Mhando amesema Karatu ndio mlango wa kuingia kwenye Hifadhi za Taifa na baada ya watalii kutoka hifadhini wanapata nafasi ya kujifunza tamaduni za Kiafrika.

Amesema wanalenga kila mwezi Septemba kila mwaka kutakua kukifanyika matamasha ya urithi 15 nchini ambayo yatakua kwenye kalenda ambayo watalii kote duniani wataweza kupanga ratiba na kuyatembelea.

Pia Soma

Advertisement
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kesho Jumapili Oktoba 20, 2019.

Chanzo: mwananchi.co.tz