Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tamasha la Remmy Ongala Jumamosi

6e474b0c3a7011767256a22551c92942 Tamasha la Remmy Ongala Jumamosi

Fri, 4 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TAMASHA la muziki la Remmy Ongala linatarajiwa kufanyika Jumamosi Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa tamasha hilo, Aziza Ongala ambaye ni mtoto wa mwanamuziki Remmy Ongala (sasa marehemu) alisema huu ni msimu wa tatu wa tamasha hilo na litapambwa na wasanii zaidi ya 100.

“Tumeanzisha tamasha hilo kwa ajili ya kuenzi Dk Remmy ili muziki wake usipotee, kutakuwa na bendi 10 na wasanii 100 wa hapa Tanzania,” alisema Aziza.

Alisema tamasha hilo ni mahususi kwa ajili ya kuenzi maisha ya Ongala kwa kutumia utamaduni halisi wa muziki wake ambao ulifanya vizuri enzi za uhai wake.

Aziza alisema wasanii kutoka sehemu mbalimbali nchini ambao wanafanya muziki wa Remmy watakuwepo ili mashabiki wake wapate burudani ya muziki wake.

“Tamasha litaanza saa 4:00 asubuhi hadi saa 8:00 usiku na kiingilio ni Sh 10,000,” alisema.

Huu ni mwaka wa 10 tangu alipofariki mwanamuziki huyo nguli Dk Remmy Ongala aliyetamba na albamu zake nne, Songs for Poor Man 1989, Mambo 1992, Sema na The Kershaw Sessions 1995.

Chanzo: habarileo.co.tz