Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tale: Ni ngumu kum-manage Diamond na Zuchu 'mtu na mpenzi wake'

Diamond Na Zuchu Ndoa Tale: Ni ngumu kum-manage Diamond na Zuchu 'mtu na mpenzi wake'

Mon, 17 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Msanii Diamond Platnumz, Hamisi Taletale maarufu kama Babu Tale amesema kuwa hakuna kazi ngumu kama kuwaongoza wasnii Diamond na Zuchu kwani wawili hao ni wapenzi.

Tale amesema kuwa, chochote ambacho unaweza kukifanya kwa mmoja anaweza kuchukulia kama unaingia mahusiano yao ya kimapenzi hivyo hata kazi yenyewe ikaharibika.

"Kumuongoza mtu na mpenzi wake, ikitokea utofauti wowote katika yao ukiingilia kwa kukurupuka inaweza kukuletea tatizo kwasababu utakuwa unaingilia furaha ya mtu.

"Nakumbuka wakati tuko Mwanza nilikuwa sitaki Zuchu aimbe kwenye shoo ya Diamond, lakini alikuja kwa mpenzi wake nikamwambia hapa umekuja kwa mpenzi wako na siyo kuimba nisikuone jukwaani, akasema sawa boss.

"Sasa ikapigwa ile nyimbo ambayo yeye na Diamond wanakumbatiana, akasema boss embu niache kwanza kidogo akapanda jukwaani wakaimba na huwezi kumkata hela, huwezi kumuadhibu kwasababu sometimes inabidi uelewe usiwe boss mnoko, ila matamanio yangu ni kuwaona wanafunga ndoa.

"Na hiyo ndio picha ambayo naiona sasa hivi kwa Diamond, watu walishaongea sana lakini mimi naona Diamond anaenda kumuoa Zuchu.

"Kuhusu kulinganishwa uzuri na ma ex wa Diamond waliopita watu waelewe kwamba kuna mahusiano na kuna furaha ya moyo, naamini pale furaha yake imefika mwisho, naiona ndoa pale," amesema Babu Tale.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live