Mtayarishaji DJ Mustard na aliyekuwa mkewe Chanel Thierry wamefikia mwisho, mchakato wa talaka yao umekamilika rasmi. Mustard amefanikiwa kubakisha mali zake ikiwemo magari yake ya kifahari na majumba. Lakini ametakiwa kulipa matunzo ya mtoto ambapo atakuwa akitoa ($24,500) zaidi ya TSh. MILIONI 66 kwa mwezi.
Mbali na pesa ya matunzo ya mtoto, Mustard ametakiwa kumlipa Chanel ($315,000) zaidi ya TSh. MILIONI 859 kama pesa ya usaidizi wa mwenza yaani Spousal Support ambayo atailipa mara moja tu na ($275,000) kama fidia ya kutogawana mali ambapo Mustard amefanikiwa kubaki na mali zake ikiwemo magari na majumba.
Wawili hao waliodumu penzini kwa miaka kadhaa, wameachana baada ya kudumu kwenye ndoa kwa mwaka mmoja na nusu tu, walifunga ndoa Oktoba 2020.