Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TOT, Makongoro wamuenzi Magufuli Mwanza

Fe405bbc3de0262c1897ad5cadc8faaa TOT, Makongoro wamuenzi Magufuli Mwanza

Thu, 25 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KATIKA muendelezo wa shughuli za kuaga mwili wa Rais John Magufuli jana kwenye jiji la Mwanza, kundi la muziki la The Tanzania One Theatre (TOT) na kwaya ya vijana ya Makongoro waliimba nyimbo za maombelezo ya kiongozi huyo wa awamu ya tano.

Shughuli ya kuaga mwili wa Rais Magufuli ilifanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba na kuhudhuriwa na wananchi wengi kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho.

Makundi hayo ya wananchi yalikuwa yakiimba ‘Nenda Magufuli’ kwa huzuni kubwa, huku wakijaribu kuelezea safari ya kiongozi huyo enzi za uhai wake kuwa wataendelea kumkumbuka.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyashukuru makundi yote yaliyojitokeza kumuenzi kiongozi huyo.

“Tunawashukuru wasanii waliokuja kutuimbia na kutufariji kwa nyimbo za maombolezo, ni kazi nzuri zimefanywa na makundi mbalimbali,” alisema. Baadhi ya wasanii walioonekana Mwanza katika shughuli hizo ni Rajabu Abdul ‘Harmonize’ akiwa na rafiki yake wa karibu Kajala Masanja.

Chanzo: www.habarileo.co.tz