Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TID mbona kila kitu tayari?

Mwanamuziki TID TID Mnyama

Mon, 27 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ulikuwa wapi mwaka 2003? Top In Dar, anatoa kichupa, akiendesha ndege angani na mrembo. Wimbo “Siamini".

Ujumbe. TID aliishi mbele ya muda. Tangu zamani hizo. Alitoa video kali. Alipendeza kimwonekano.

TID ni wa kwanza Bongo Flava kuamini katika kuwekeza kwenye video bora. Alisafiri visiwani na nje ya mipaka kufuata location zenye kuvutia.

Tafsiri package. Sauti nzuri, tungo bomba, tukapata muziki mzuri. Video kali, mpangilio mzuri wa mavazi. Jukwaani shoo alifunika kwa kuimba na kudance.

Handsome. Ndio sifa ya TID iliyovuma. Wadada walimwita sukari. TID akawa ndoto ya kila mrembo aliyetamani kudate mwanaume superstar.

Ukiona watoto wadogo wanashobokewa na warembo. Kaa ukijua kuwa TID alisakwa. Warembo walimpenda sana Top In Dar.

Sumaku ya TID kwa wadada wa mjini ilikuwa na mchanganyiko wa sifa nyingi ndani ya mtu mmoja; muziki mzuri, sauti maridadi, walimwita handsome, aliendesha magari mazuri, alipanda sana ndege, na alimiliki fedha katika umri mdogo.

Mwanasanaa kamili. Miaka 17 imepita. TID alipanda jukwaani, Diamond Jubilee, Upanga, akiwa na mabegi. Alikuwa mbichi kabisa akitokea UK. Sio Ukonga wala Ukerewe. Ni United Kingdom. Mngejuaje kama Mnyama wa Kino alitoka Ulaya?

Zamani hizo, TID alifanya u-MC wa matukio na watu walimpenda. Wakadhani hicho ndicho kipande alichoandikiwa na Mungu. Alipata nafasi redio ya utangazaji.

Sauti, vionjo na ubunifu, vikafanya apendwe. Watu wakatabiri kuwa angefika mbali kwenye utangazaji.

Alipotoa nyimbo mfululizo, wadau wakakiri muziki ndio kipaji halisi cha TID. Movie ya Girlfriend, ilipoleta mapinduzi makubwa katika soko la filamu, maoni yakapendekeza kuwa TID afanye muziki kidogo halafu aigize zaidi. Siku hizi amekuwa mwingi wa comedy. Wengi wanamshauri afanye comedy.

Tafsiri. Tangu virasta, bleach mpaka kokoto, TID ni binadamu pendwa katika angle nyingi.

Twende Alliance Francaise, Upanga, leo. TID ataheshimishwa kupitia platform ya Bongo Flava Honors. Sugu atahost shughuli. Tutamjua TID nje ndani. Halafu atatuhudumia kwa shoo ya saa mbili jukwaani.

Anastahili. Mtanzania yuleyule wa pekee. Mwenye sauti ya pekee. Sauti ya Dhahabu. Ndimi Luqman MALOTO

Chanzo: www.tanzaniaweb.live